9. Maisha, Mauti na Ufufuo wa Kristo
Katika maisha ya Kristo ya utii mkamilifu kwa mapenzi ya Mungu, mateso yake, mauti na ufufuo, Mungu alitoa njia pekee ya kafara kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu, ili kwamba wale ambao kwa imani wanapokea upatanisho huu waweze kuelewa vizuri zaidi upendo mtakatifu usio na kikomo wa Muumbaji. Kafara hii kamilifu huthibitisha haki ya sheria ya Mungu na fadhili za tabia yake; kwa sababu hufanya vyote viwili kuhukumu dhambi yetu na kutupatia msamaha. Kifo cha Kristo ni cha badala na cha kulipia, kupatanisha na chenye kubadilisha. Ufufuo wa Kristo hutangaza ushindi wa Mungu dhidi ya nguvu za uovu, na kwa wale wanopokea kafara huhakikisha ushindi wao wa mwisho dhidi ya dhambi na mauti. Kinatangaza ukuu wa Yesu Kristo, ambaye mbele zake kila goti mbinguni na duniani litapigwa
Mafungu ya Biblia
Yoh. 3:16; Isaya 53:1; IPet. 2:21, 22; IWakor. 15:3, 4, 20 – 22; IIWakor. 5:14, 15, 19 – 21; Warumi 1:4; 3:25; 4:25; 8:3, 4; IYoh 2:2; 4:10; Wakol. 2:15; Wafilipi 2: 6 – 11
