28. Dunia mpya
Katika dunia mpya, ambamo haki hukaa, Mungu ataweka tayari makao ya milele kwa waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa maisha ya milele, upendo, furaha na kujifunza mbele zake. Kwa kuwa hapa Mungu Mwenyewe atakaa pamoja na watu wake, na taabu na mauti vitakuwa vimepita. Pambano kuu litakuwa limemalizika, na dhambi haitakauwako tena. Vitu vyote, vyenye uhai na visivyo na uhai vitatangaza kwamba Mungu ni pendo; naye atatawala milele. Amina
Mafungu ya Biblia
IIPet. 3:13; Isaya 35; 65:17 – 25; Math. 5:5; Ufun. 21:1 – 7; 22:1 – 5; 11:15
