15. Ubatizo
Kwa njia ya ubatizo tunakiri imani yetu katika kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, na kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi letu la kuenenda katika upya wa maisha. Hivyo tunamkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi, tunakuwa watu wake, na tunapokelewa kama washiriki na kanisa lake. Ubatizo ni mfano wa muungano wetu pamoja na Kristo, msamaha wa dhambi zetu, na kupokea kwetu Roho mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa majini na unategemea uthibitisho wa imani katika Yesu na ushahidi wa toba ya dhambi. Unafuatia mafunzo katika Maandiko Matakatifu na ukubali wa mafundisho yake
Mafungu ya Biblia
Warumi 6:1 – 6; Wakol. 2:1,2,13; Mdo. 16:30 33; 22:16; 2:38; Math. 28:19, 20
