6. Uumbaji
Mungu ni Muumba wa vitu vyote, na amefunua katika Maandiko uhalisi wa tukio la shughuli zake za uumbaji. Katika siku sita Bwana alizifanya “mbingu na nchi” na vitu vyote vilivyo hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba ya juma lile la kwanza. Na hivyo akaanzisha Sabato kama kumbukumbu ya milele ya kukamilika kwa kazi yake ya uumbaji. Mwanamume na mwanamke wa kwanza walifanywa kwa mfano wa Mungu kama upeo wa kazi yake ya uumbaji, wakapewa utawala juu ya ulimwengu, na wakaagizwa kuwajibika na utunzaji wake. Wakati ulimwengu ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ni chema sana,” ukitangaza utukufu wa Mungu
Mafungu ya Biblia
Mwa. 1:2; Kut. 20:8 – 11; Zab. 19:1 – 6; 33:6, 9; Waeb11:3
