26. Mauti na Ufufuo
Mshahara wa dhambi ni mauti. Lakini Mungu, ambaye peke yake hapatwi na mauti, atawapa uzima wa milele waliokombolewa wake. Mpaka siku hiyo mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu kwa watu wote. Wakati Kristo, aliye uzima wetu atakapotokea, wenye haki waliofufuliwa na wenye haki walio hai watavikwa utukufu na kunyakuliwa juu ili kumlaki Bwana wao. Ufufuo wa pili ni ufufuo wa waovu, utatokea miaka elfu moja baadaye
Mafungu ya Biblia
Warumi 6:23; I Tim. 6:15, 15; Mhu. 9:5, 6; Zab. 146:3, 4; Yoh. 11:11 – 14; Wakol. 3:4; IWakor. 15:51 – 54; IWathes. 4:13 – 17; Yoh. 5:28, 29; Ufun. 20:1 – 10
