20. Sabato
Muumbaji mkarimu, baada ya siku sita za uumbaji, alipumzika siku ya saba na kuanzisha Sabato kwa ajili ya watu wote kama kumbukumbu ya uumbaji. Amri ya nne ya sheria za Mungu zisizobadilika inaagiza adhimisho la Sabato hii ya siku ya saba kama siku ya mapumziko, ibada, na huduma kulingana na mafundisho na uzoefu wa Yesu, Bwana wa Sabato. Sabato ni siku ya mawasiliano yenye furaha pamoja na Mungu na sisi kwa sisi. Ni mfano wa ukombozi wetu katika Kristo, ishara ya utakaso wetu, ishara ya utii wetu, na mwonjo wa umilele wetu wa siku zijazo katika ufalme wa Mungu. Sabato ni ishara ya daima ya Mungu ya agano la milele la Mungu kati yake na watu wake. Utunzaji wa furaha wa wakati huu mtakatifu toka jioni hadi jioni, jua kuchwa hadi jua kuchwa, ni adhimisho la matendo ya Mungu ya uumbaji na ukombozi
Mafungu ya Biblia
Mwa. 2:1 –3; Lut. 20:8 – 11; Luka 4:16; Isaya 56:5, 6; 58:13, 14; Math. 12:1 – 12; Kut. 31:13 – 17; Ezek. 20:12, 20; Kumb. 5:12 – 15; Waebr. 4:1 – 11; Walawi 23:32; Marko 1:32
