P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 4

Mwana

4. Mwana

Mungu Mwana wa milele alifanyika mwili katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote viliumbwa, tabia ya Mungu imefunuliwa, wokovu wa wanadamu unakamilishwa na ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu aliye Kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira Mariamu. Akaishi na kupitia uzoefu wa majaribu kama mwanadamu, lakini kwa ukamilifu alionyesha kwa mfano haki na upendo wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama Masihi aliyeahidiwa. Aliteseka na kufa kwa hiari msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kuhudumu katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika utukufu kwa ajili ya ukombozi wa mwisho wa watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote

Mafungu ya Biblia

Yoh. 1:1 – 3, 14; Wakol. 1:15 – 19; Yoh. 10:30; Wafil. 2:5 – 11; Waebr. 2:9 – 18; IWakor. 15:3, 4; Waebr. 8:1, 2; Yoh. 14:9; Warumi 6:23: IIWakor. 5:17 – 19; Luka 1:35; Yoh. 14:1 – 3