25. Kuja kwa Kristo mara ya pili
Kuja kwa Kristo mara ya pili ndilo tumaini lenye baraka la kanisa, hitimisho kuu la injili. Kuja kwa Mwokozi kutakuwa halisi, binafsi, kutakakoonekana, na kwa dunia nzima. Atakaporudi, wenye haki waliokufa watafufuliwa na pamoja na wenye haki walio hai watavikwa utukufu na kuchukuliwa kwenda mbinguni, lakini waovu watakufa. Kutimizwa karibu kabisa kwa sehemu nyingi za unabii pamoja na hali ya sasa ya ulimwengu, huonyesha kwamba kuja kwa Kristo ku karibu sana. Wakati wa tukio hilo hakukufunuliwa, na hivyo basi tunahimizwa kuwa tayari kwa nyakati zote
Mafungu ya Biblia
Tito 2:13; Waebr. 9:28; Yoh. 14:1 – 3; Mdo. 1:9 – 11; Math. 24:14; Ufun. 1:7; Math. 24:43, 44; IWathes. 1: 7 – 10; 2:8; Ufun. 14:14 – 20; 19:11 – 21; Math. 24; Marko 13; Luka 21; IITim. 3:1 – 5; IWathes. 5:1 – 6
