P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 23

Ndoa na Familia

23. Ndoa na Familia

Ndoa ilianzishwa na Mungu katika Edeni na ikathibitishwa na Yesu kuwa muungano wa maisha yote kati ya mwanamume na mwanamke katika wenzi wenye upendo. Kwa Mkristo kifungo cha ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi, na kishirikiwe tu na wenzi wenye imani moja. Upendo wa hiari, heshima, staha, na uwajibikaji ndizo fito za (kujengea) uhusiano huu, ambao utaakisi upendo, utakatifu, ukaribu, uthabiti wa uhusiano kati ya Kristo na kanisa lake. Kuhusu talaka, Yesu alifundisha kwamba mtu anayemwacha mwenzi, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, na akaoa (au kuolewa) na mwingine, azini. Ingawa baadhi ya mahusiano ya kifamilia huenda yakashindwa kufikia lengo, wenzi katika ndoa ambao wamejitoa kikamilifu kila mmoja kwa mwenzake katika Kristo wanaweza kufaulu kufikiliza katika umoja wenye upendo kupitia uongozi wa Roho Mtakatifu na malezi ya kanisa. Mungu hubariki familia na anakusudia kwamba washirika wake watasaidiana wao kwa wao kufikia upevu kamili. Wazazi wawalee watoto wao katika kumpenda na kumtii Bwana. Kwa kielelezo chao na maneno yao wawafundishe kwamba Kristo ni mtiishaji mwenye upendo, daima mpole na mwenye kujali, anayetaka wawe viungo vya mwili wake, familia ya Mungu. Kukuza ukaribu wa uhusiano wa kifamilia ni mojawapo ya alama (ya kujulisha) ujumbe wa mwisho wa injili

Mafungu ya Biblia

Mwa. 2:18 – 25; Math. 19:3 – 9; Yoh. 2:1 – 11; IIWakor. 6:14; Waef. 5:21 – 33; Math. 5:31, 32; Marko 10:11, 12; Luka 16:18; IWakor. 7:10, 11; Kut. 20:12; Waef. 6:1 – 4; Kumb. 6:5 – 9; Mith. 22:6; Malaki 4:5, 6