P.O. Box 346, Dodoma, Tanzania Sabato: 8:00 AM – 1:00 PM
Imani ya 5

Roho Mtakatifu

5. Roho Mtakatifu

Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji, kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa Maandiko Matakatifu, alijaza maisha ya Kristo na uwezo. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu; na wale wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa, huliwezesha kumshuhudia Kristo, na kwa upatano na Maandiko huliongoza kwenye ukweli wote

Mafungu ya Biblia

Mwa. 1:2; Luka 1:35; 4:18; Mdo. 10:38; IIPet. 1:21; IIWakor. 3:18; Waef. 4:11, 12; Mdo. 1:8; Yoh. 14:16 – 18, 26; 15:26, 27; 16:7 – 13