13. Masalio na Utume Wake
Kanisa la ulimwengu linajumuisha wale wote ambao kwa kweli wanamwamini Kristo, lakini katika siku za mwisho, kipindi cha kuenea kwa ukengeufu, masalio wameitwa kuzishika amri za Mungu na imani ya Yesu. Masalio hawa hutangaza kuwadia kwa saa ya hukumu, hutangaza wokovu kupitia kwa Kristo, na hupiga mbiu ya kukaribia kwa marejeo yake. Tangazo hili huwakilishwa katika mfano wa malaika watatu wa ufunuo 14; huambatana na kazi ya hukumu mbinguni na kuwa na matokeo ya kazi ya toba na matengenezo duniani. Kila muumini anatakiwa kuwa na sehemu binafsi katika ushuhuda huu wa ulimwenguni kote
Mafungu ya Biblia
Ufun. 12:17; 14:6 – 12; 18:1 – 4; IIWakor. 5:10; Yuda 1:3, 14; IPet. 1:16 – 19; IIPet. 3:10 – 24; Ufun. 21:1 – 14
