3. Baba
Mungu Baba wa milele ndiye Muumbaji, chimbuko, Mtegemezaji, na Mfalme wa viumbe wote. Ni mwenye haki na Mtakatifu, mwingi wa rehema, mwenye fadhili, si mwepesi wa hsira, ni mwingi wa uthabiti wa upendo na uaminifu. Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni ufunuo wa Baba
Mafungu ya Biblia
Mwa. 1:1; Ufun. 4:11; IWakor. 15:28; Yoh. 3:16; IYoh. 4:8; ITim. 1:17; Kut. 34:6, 7; Yoh. 14:9
