1. Maandiko Matakatifu
Maandiko Matakatifu yaani Agano la Kale na Jipya ndiyo neno la Mungu lililoandikwa likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia kwa watu watakatifu wa Mungu walionena na kuandika kama walivyoongozwa na Roho Mtakatifu. Ndani ya Neno hili, Mungu amemkabidhi mwanadamu maarifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu. Maandiko Matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa wa mapenzi yake. Ndiyo upeo wa tabia, kipimo cha uzoefu, ufunuo thabiti wenye mamlaka wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu aminifu ya matendo ya Mungu katika historia
Mafungu ya Biblia
IIPet.1:20, 21; IITim. 3:16, 17: Zab. 119:105l Mith. 30:5, 6; Isa. 8:20; Yoh. 17:17; IWathe. 2:13; Waeb. 4:12
